Chama cha madaktari Tanzania (MAT) kimeiomba serikali kuwahakikishia madaktari na wauguzi vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona (Covid 19) ili wasipate maambukizi pindi wanapowahudumia wagonjwa wenye virusi hivyo.

Rais wa chama hicho, Dkt. Elisha Osati akizungumza na waandishi wa habari amesema vifaa vya kujikinga ni muhimu kwao ikizingatiwa idadi ya wagonjwa waliokatika hatari ya kupata maambukizi inaongezeka siku hadi siku

Aidha, ameishauri serikali kupunguza msongamano katika kliniki za magonjwa mengine kama kisukari na ukimwi kwa kutoa dawa za muda mrefu.

”Kwa mfano wagonjwa wale wa kisukari shinikizo la damu, maumivu migongo na misuli wanaweza kupewa dawa walau ya miezi mitatu kwaasababu hawa wanauwezekano wa kupata ugonjwa makali zaidi,” amesema Dkt Osati

Katika hatua nyingine ameipongeza serikali kupitia ofisi ya Waziri mkuu na wizara ya afya kwa namna wananvyoongoza nchi kupambana ugonjwa huo.

CORONA: Mwanasiasa ajitetea kumtusi Ronaldo
Tanasha afunguka uhusiano ‘mgumu’ na Mama Diamond, sababu za kuachana

Comments

comments