Madaktari wawili wataalam wa upasuaji katika hospitali moja binafsi jijini Lagos nchini Nigeria, wamejikuta wakibanwa na sheria kwa kusababisha kifo cha mgonjwa baada ya kusahau taulo ndani ya tumbo lake.

Taarifa iliyoripotiwa na PM News, imewataja madaktari hao kuwa ni Dk. Taiwo Shogule (53) na Dk. Adeleke Olusegun (43), wote wataalam wa hospitali ya St. Raphael Divine Mercy ya Ijede, Ikorodu jijini humo.

Madaktari hao walikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo walisomewa mashataka ya uzembe kazini na mauaji ya mgonjwa, Omojola Bamgboye.

Mwendesha mashataka, Supol Eshiet Eshiet aliiambia Mahakama kuwa madaktari hao walitenda kosa hilo kati ya Desemba 18 na 19 mwaka 2015, na kwamba kutokana na uzembe wao, walimuua mgojwa kwa kusahau taulo kwenye utumbo wa mgojwa.

Hata hivyo, washtakiwa wote walikana mashtaka dhidi yao na walipewa dhamana kwa mashati magumu wakitakiwa kurudi mahakamani hapo Septemba 9 mwaka huu.

Breaking News: Ndege ya Emirates yaanguka ikiwa na abiria 275
Tundu Lissu awaka, avutana na agizo la Rais