Msanii wa nyimbo za injili Madam Flora ametoa onyo kali kwa watu waliozoea kumzushia story za uongo na amesema sheria itachukua mkondo wake.

”Na niseme tu kwamba hivi sasa sitakaa kimya tena, huyo aliyezoea kunizushia story za uongo akifikiri siijui sheria ajipange vizuri maana Mahakama ipo na sheria ipo” amesema Madam Flora.

Siku chache zilizopita taarifa zilizagaa mitandaoni zikidai kuwa Madam Flora amezungumza amesema aliachana na mume wake kisa haridhishwi kinyumba.

Leo Madam Flora amehojiwa na chombo kimoja cha habari na kukanusha madai hayo yaliyozungumzwa juu ya kuvunjika kwa ndoa yake.

Madam Flora amethubutu kusema ni uzushi mtupu na hayana ukweli wowote.

Hizi habari ni za uongo, sijafanya mahojiano na radio yoyote na kuzungumza maneno hayo, naomba mzipuuze maana ni mpuuzi mmoja tu ameamua kuonyesha upuuzi wake na kutafuta followers kwenye page yak” amesema Madam Flora.

Aidha amewambia wabaya wake kuwa anaijua sheria hivyo wakae chonjo na wajipange kupambana nayo.

 

Dida Ajirudisha Young Africans
Craig Shakespeare Awakaribisha AS Roma