Serikali imewaagiza Wahandisi wa Mamlaka ya Barabara za mjini na vijijini TARURA kuzunguka nchi nzima kukagua madaraja yote ambayo yameharibika ili yaweze kurekebishwa na kujengwa.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa daraja la iwelengula Wilaya ya Shinyanga ambalo linajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 428, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, David Silinde amesema kuwa ukarabati wa madaraja utasaidia kuunganisha tena vijiji vilivyokuwa vimekosa mawasiliano kwa kuaharibika kwa miundombinu na kuendelea kupata huduma mbalimbali za kijamii.

Ametolea Mfano kijiji cha iwelengula baada ya wananachi wa mtaa wa iwelengula kukosa mawasiliano kutokana na mvua kali zilizotokea mwanzoni mwa mwaka huu na kupelekea wananchi hao kushindwa kupata huduma mbalimbali za kijamii maeneo mengine kwa urahisi.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ameishukuru TAMISEM kupitia TARURA kwa kujenga daraja hilo kwa haraka kwani wananchi walikuwa wanateseka kupata huduma hasa za afya, daraja hilo lilikua linaunganisha wananchi wa kata mbili tofauti ambao wanategemeana katika huduma mbalimbali.

Naye Meneja wa TARURA Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi amesem ujenzi wa daraja kwa sasa umefikia hatua nzuri itakapofika mwezi wa tisa litakuwa linapitika vizuri, ingawa limechelewa kuanza kujengwa kutokana na sababu za kiufundi ambao baadhi ya vifaa kuchelewa kufika kutoka kiwandani na maji kua mengi eneo hilo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii afanya ziara Tendaguru
Wafariki kwa kulala na jiko la mkaa ndani