Siku chache baada kusambaa kwa sauti ya Dogo Janja akimshawishi msichana amkubali huku akiporomosha lawama na vijembe kwa Uongozi wa Tip Top pamoja na Madee kuwa wamemrudisha kundini ili kumuua kimuziki, Madee ameeleza kinachojiri upande wao.

Akiongea jana na Clouds Fm, Madee alieleza kushangazwa na kauli alizosikia kwenye mazungumzo ya simu kati ya Dogo Janja na mrembo huyo nakueleza kuwa hafahamu kwanini aliamua kuyasema hayo ikiwa ni siku moja baada ya kukamilika kwa wimbo wake mpya na video.

“Haya maneno yanayoongelewa kwenye hiyo voice note, mimi jana (juzi) usiku tu nimetoka kumaliza kazi ya Dogo Janja kwa Master Jay na nikawa najiuliza mara mbilimbili, ‘hii kweli ni sauti yake au sio’. Lakini sasa kwa upande mwingine nikawa nashindwa kuwa na maamuzi yote kwa sababu Tip Top ina menejimenti yake,” alisema Madee.

Alieleza kuwa wakati anasikiliza sauti hiyo, Babu Tale alikuwa nje ya nchi akifanya kazi na Diamond na wengine hivyo asingeweza kujadiliana nao au kufanya maamuzi yake binafsi.

Ingawa Madee anaeleza kukwazwa na sauti hiyo, lakini ana mawazo chanya ya kufikiria mazingira ya mazungumzo kati ya Dogo Janja na msichana huyo aliyekuwa anamtongoza.

“Nilikuwa naogopa kumuattack Dogo Janja moja kwa moja kwa sababu ukifuatilia kwa haraka haraka unagundua kwamba alichokuwa anajaribu kukipata ni yule mwanamke ambaye alikuwa anajaribu kumdanganya. Pia nikatumia akili yangu ya kawaida kwamba muda mwingine huwa tunajaribu kudanganya sana tukiwa tunatongoza ili tufanikishe kile ambacho tunakitaka,j” alieleza.

Hata hivyo, Madee alikiri kuwa kwa upande mwingine Dogo Janja anaonekana ana kitu ambacho anacho moyoni.

Naye Dogo Janja ameeleza kuwa anaendelea na juhudi za kumtafuta Madee ili waweze kuzungumza lakini hajafanikiwa kwani akimpigia simu hapokei. Alisema walikutana Ikulu kwenye hafla iliyoandaliwa kuwashukuru wasanii kwa kufanikisha kampeni za Rais John Magufuli lakini hakufanikiwa kuzungumza naye.

 

Donald Trump awashawishi watu kuigomea Apple
Utapenda majibu ya Bushoke kwa shabiki aliyetaka kujua lini atafika ‘level’ za Diamond