Madereva wa pikipiki maarufu ‘bodaboda’ na madereva bajaji wamelalamikia tabia ya baadhi ya askari kuwalazimisha kulipa fedha pasipo makosa na kuwabambikizia makosa ambayo hawajayatenda.

Wakizungumza kupitia kipindi cha Sauti zetu kinachoruka Dar24, madereva hao kuwa kuna baadhi ya makosa wanayafanya kutokana na hali ya hofu ya kukamamtwa kwa kuwa wakati mwingine wanapokamatwa hutafutiwa kosa na kulazimishwa kuwapatia pesa mapolisi, na wanapokataa kuwapa fedha hutafutiwa makosa.

Wametoa malalamiko hayo ikiwa ni siku chache baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene kutoa agizo kwa maaskari kuacha mara moja kutumia nguvu wakati wa kuwakamata madereva bodaboda na bajaji barabarani kwa kuwa hali hiyo inahatarisha maisha.

Mtoto wa darasa la tatu afariki akiigiza watu wanavyojinyonga

Madereva hao wamesema licha ya uzuri wa agizo hilo la Waziri, lakini utekelezaji huenda ukawa mgumu kwani kuna wakati inawalazimu kuvunja sheria ili kujisaidia na wanapofanya kinyume na matakwa ya askari hao, ni lazima wawe na kiasi kikubwa cha fedha kulipa faini ya makosa wanayotafutiwa.

Aidha, wamelalamikia tabia ya kukimbizwa na askari kama majambazi na wakati mwingine baadhi ya maaskari kuwavizia madereva bodaboda na kuchomoa funguo za pikipiki kabla ya kukagua iwapo wana makosa au la.

Hata hivyo Madereva hao wameshauriana wao kwa wao kujitahidi kufuata sheria lakini kwa upande wa askari kuacha kutumia nguvu kuwakamata.

Mapema wiki hii, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene alitoa agizo kwa kwa maaskari kuacha mara moja kutumia nguvu wakati wa kuwakamata madereva Bodaboda na bajaji barabarani kwakuwa hali hiyo inahatarisha maisha.

GSM: Manji anakaribishwa Young Africans
ASFC kuendelea April 28