Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amewataka madereva wa bodaboda na bajaji kutoshiriki katika maandamano yasiyo na vibali vya polisi.

Mutafungwa, amesema kampeni za uchaguzi mkuu zimeanza maeneo mbalimbali nchini na kuwataka madereva hao kuendelea na kazi zao bila kushiriki maandamano.

“Hakikisheni hamshiriki maandamano ya kisiasa ambayo hayana kibali maalumu kutoka polisi kwani kufanya hayo ni kinyume cha sheria, kwa sababu watawanunulia mafuta lita moja kisha mkajiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa sheria,” amesema Mutafungwa.

Aidha, amesema kuwa ni vizuri madereva hao wakafanya kazi kwa mujibu wa sheria

Keita aachiwa huru, Mali kuunda serikali ya mpito
Viongozi wawasili Ukerewe kudhibiti mauaji