Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma Trafiki Makao Makuu, Mossi Ndozero, amewataka madereva wa magari ya serikali kuzingatia matumizi sahihi na salama ya barabara ikiwa kufuata sheria, michoro na ishara za barabarani ili kupunguza ajali.

Kwa mujibu wa Gazeti la Nipashe Ndozero, amesema madereva wote wa Serikali wanaomiliki leseni wako kwenye kundi moja la kutii sheria na kanuni za usalama barabarani, hivyo wasijione wapo juu ya sheria.

Jeshi hilo limeonya kuwa ikitokea wamekamatwa wakiwa wamevunja sheria, wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kama madereva wengine.

Mossi Ndozero, amesema kuwa kumeibuka wimbi kubwa la matukio ya madereva wa magari ya serikali kuvunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi wakifikiri kuwa wao hawaguswi.

Aweso atoa siku 30 wananchi wapate maji Handenife
Maaskari waliouawa kwenye shambulio la risasi Dar waanga leo