Kufuatia kukithiri kwa ajali za barabarani hali iliyompelekea rais Magufuli kutamka amechoshwa na kutuma rambirambi pamoja na salamu za pole kwa wafiwa na majeruhi, Waziri wa Mambi ya Ndani Kangi Lugola amekuja na mikakati mbalimbali kuhakikisha ajali za hizo zinakoma.

Ambapo kuanzia sasa ajali yeyote ya gari itakayotokea na kubainika kuwa imesababishwa na ubovu wa gari, Lugola ametangaza dereva wa gari hiyo pamoja na mmiliki wake bila kujali nafasi yake, nguvu aliyonayo kiuchumi watafikishwa mahakamani na kulazwa mahabusu

Amesema dereva atafikishwa mahakamani kwa kosa la kuendesha gari bovu, lakini pia mmiliki wake atafikishwa mahakamani kwa kuruhusu gari bovu kuendeshwa barabarani mpaka kusababisha ajali.

Ameongezea kuwa wawili hao lazima walale mahabusu ya polisi na kutoa onyo kali endapo atagundua dereva na mmiliki wake watafikishwa mahakamani pasipo kufikishwa mahabusu atakayehusika na kesi hiyo atapata tabu sana.

Aidha Waziri Lugola amekwisha tekeleza baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na kuvunja baraza la usalama wa barabarani taifa pamoja na kamati zake zote mikoani na wilayani ili kuunda baraza jipya ambalo linategemewa kuwa tayari limekamilika mpaka ifikiapo mwisho wa mwezi huu.

”Nataka niwahakikishie watanzania tumeanza kuweka mikakati madhubuti mikakati yenye hatua kali kwa wale wote ambao watasababisha ajali za barabarani na moja nilianza kwa kuvunja baraza la usalama barabaarani la taifa na kamati zake mikoani na wilayani baada ya kubaini  kuna mapungufu mkubwa katika kudhibiti ajali barabarani.

Nataka kuwahakikishia watanzania baraza hili mpaka kufika mwisho wa mwezi huu baraza hilo litakuwa limeundwa na kutangazwa ili kutoa fursa sasa kwa kamati za usalama barabarani za mikoa na wilaya na zenyewe sasa kuundwa”amesema Lugola.

 

 

Picha: Rais Magufuli akitoa salamu za pole familia ya Kikwete
Lugola aagiza wafungwa kuanza kujilisha

Comments

comments