Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani, Fortunatus Musilimu amesema kuwa dereva yeyote atakayebainika kuwa na leseni bila cheti cha shule au chuo alikosoma leseni yake itazuiwa hadi pale atakapoleta vyeti kuthibitisha chuo au shule alikosomea udereva.

Ameongezea kuwa dereva huyo atakuwa amekosa sifa za kuwa dereva na leseni yake itafungiwa kwani atakuwa amepata leseni hiyo katika utaratibu usiokubalika kwa mujibu wa sheria.

”Madereva watakaokuwa na leseni bila vyeti vya shule walilkosoma tutazuia na tutazichukua leseni zao lakini pia watalazimika kwenda darasani kusoma wakishamaliza kusoma tutawafanyia utahini na wale watakaofaulu tu ndio tutawarejeshea leseni zao wale ambao hawatafaulu watarudi darasani kusoma”. amesema Musilimu.

Musilimu amesema hayo leo Julai 24, 2018 alipokuwa akitoa ripoti juu ya utaratibu mpya unaotarajiwa kuanzishwa katika zoezi zima la uhakiki wa leseni kwa njia ya kielektroniki ambapo katika kampeni iliyoanzishwa julai 4 mwaka huu ajali zimepungua kwa kiasi chake kulinganisha na mwezi uliopita na hata hivyo idadi kubwa ya madereva wamekutwa na makosa hivyo kikosi cha usalama kimedhamiria kufanya uhakiki wa madereva nchi nzima ili kuhakikisha madereva wanakuwa makini na mahiri kusaidia kuhakikisha ajali barabarani zinazotokana na uzembe zinapungua.

Hata hivyo jumla ya leseni 73904 za madereva zimakaguliwa na madereva 878 walibainika kuendesha magari kwa kutumia leseni zenye madaraja yasiyostahili, leseni 1808 zimepatikana kutumika ikiwa muda wake umekwisha, na madereva 173 wamefikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali.

Aidha, amesema kuwa madereva wote watakaobainika kuendesha magari bila leseni stahiki kulingana na magari yanayoendeshwa watakamtwa na kutiwa mahubusu kisha kupandisha mahakamani.

 

Kesho Waziri Mkuu kuongoza zoezi la usafi Coco beach
Juventus kumrudisha Bonucci, Higuain afanywa chambo

Comments

comments