Siku hizi imezuka fasheni ya watu kupendelea zaidi kutumia ‘earphone’ spika za masikioni kwa kuongea na simu, kusikiliza muziki na matumizi haya ya earphone humsaidia mtu kupata uwezo wa kufanya shughuli zake nyingine.

Ukweli ni kwamba kusikiliza muziki wa sauti ya juu kwa kutumia spika za masikioni kuna athari kubwa ambazo mtu anaweza kuzipata hapo baadae.

Wataalamu wa mambo haya walifanya tafiti zao na kugundua kuwa usikilizaji wa sauti ya juu au sauti kubwa kwa kutumia spika za masikioni kuna weza pelekea mtu kupata ukiziwi, na hatari hii ipo sana sana kwa watoto na vijana ambao tayari kundi lililoathirika na matumizi haya mabaya ya spika za masikioni

Sauti hupimwa kwa kutumia skeli ijulikanayo kama decibel (DB) mfano mtu anayeongea kwa sauti ya chini ni kadirio la 39DB.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO), kupitia takwimu zao zinaonesha kuwa miongoni mwa wale walio na umri wa miaka 13 hadi 35 yaani asilimia 50 husikiliza sauti katika kiwango kisicho salama.

Shirika la Afya (WHO) limeainisha kuwa kukaa eneo lenye kiwango cha sauti kuanzia 85DB kwa masaa nane au 100DB kwa dakika 15 siyo salama.

Inakadiriwa kuwa walio chini ya miaka 20 ni vijana ambao wapo katika hatari ya kupoteza usikivu kutokana na matumizi ya vifaaa vya sauti zikiwemo simu zao.

Hivyo inashauriwa kiwango cha juu cha sauti katika maeneo ya kazi ni 85DB  bila kuzidi saa nane.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 20, 2019
Madhara ya utumiaji wa spika za masikioni

Comments

comments