Kama wewe ni mvaaji wa viatu bila soksi tambua kwamba unajiweka kwenye hatari kubwa zaidi kuliko kunuka miguu peke yake.

Chuo cha tiba ya miguu nchini Uingereza kimesema kumekuwa na ongezeko la maradhi ya miguu huku mtaalamu Emma Stephenson akisema amekuwa akipokea vijana wa kati ya miaka 18-25 walio na matatizo kwenye miguu yao ambayo yametokana na kutovaa soksi au kuvaa viatu visivyowatosha vyema.

Kutovaa soksi siku hizi umekuwa mtindo maarufu wa mavazi ambapo vijana wengi katika maonesho ya mitindo pia mara nyingi huonesha mavazi wakiwa na viatu bila soksi.

Kwa kawaida miguu hutoa kiasi cha jasho cha 0.28 ya lita moja kila siku na hivyo unyevu mwingi na joto hilo husababisha muwasho na michubuko ambayo huleta magonjwa ya ngozi ya miguu.

Inashauriwa kutovaa viatu bila soksi kwa muda mrefu na kama ukuvaa bila soksi basi jaribu pia kuweka kitu cha kukausha jasho kwenye soli ya kiatu chako kabla ya kukivaa bila soksi.

TFF yatawatoa makocha katika mabenchi
Walioterekeza wazazi kusakwa mkoani Songwe