Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema atatangaza zoezi la uhakiki wa Madhehebu ya Dini yaliyomo ndani ya Mkoa wa Mbeya ili kuyafungia yale madhehebu ambayo yanakiuka taratibu na Sheria.

Inatajwa kuwa hadi kufikia 2017 Mbeya ilikuwa inaongoza kwa kuwa na madhehebu mengi zaidi nchini Tanzania yapatayo 450 ya dini za aina mbalimbali.

Lakini pia kwa takwimu hizo Chalamila amesema pia jiji la Mbeya linakadiriwa kuwa la pili Afrika kwa kuwa na Madhehebu mengi lakini bado ni miongoni mwa Majiji yenye matukio mengi ya ajabu.

  • Mchungaji amuua mkewe wakati wa ibada, naye ajichinja

Hivyo ametangaza rasmi hivi karibuni kufanya uhakiki wa madhehebu ili kujua kama yanafuata sheria na yale ambayo yatakuwa yanaendeshwa kinyume na sheria kufungiwa kwani tayari ameanza kupokea malalamiko ofisini kwake kuwa yapo madhehebu ambayo yanakiuka taratibu jambo ambalo linahatarisha amani na utulivu ndani ya mkoa huo.

Kwani kumekuwa na matukio mengi ya kikatili na kutisha ambayo yameacha kumbukumbu mbaya kwa watanzania na jamii nzima.

Mbali na kuwepo kwa madhehebu aina mbalimbali Mbeya ndio mkoa uliogubikwa na matukio ya ajabu.

Ambapo kipindi cha miaka 15 iliyopita vyombo vya habari vimeripoti matukio mengi ya kutisha baadhi ya matukio hayo ni kama binadamu kuchunwa ngozi, wapiga nondo, mauaji ya watoto chini ya miaka mitano, watu kuzikwa wakiwa hai, kukatwa sehemu za siri, kuungua kwa masoko, kituo cha maombezi kuwapora mali waumini wake, kuzika jeneza tupu na kadhalika.

Hivyo uwepo wa madhehebu mengi umepelekea kugeuza imani za watu kama biashara makanisa yametumiaka kama biashara badala ya sehemu ya kujenga imani za watu kwa kukemea matukio hayo amabyo yamekuwa yakitikisa nchi.

Aidha, suala lililoibuliwa na Mkuu wa Mkoa, Chalamila huenda likiwa muarobaini kwa madhehebu ambayo yamekuwa yakipandikiza imani potofu kwa waumini na kuwageuza kuwa mtaji.

Mfumo wa malipo kwa matokeo kuendelea kuimarisha huduma za maji vijijini
Baba kizimbani kwa kukeketa watoto wake