Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Siha, limewasimamisha madiwani wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuhudhuria vikao vya baraza hilo hadi Juni mwaka 2019.

Madiwani hao wanadaiwa kuvunja kanuni ya 10 (d), kwa kuvua joho ambalo ni vazi maalumu lililochaguliwa na madiwani wa halmashauri hiyo kwa ajili ya mikutano ya baraza na hata walipotakiwa na mwenyekiti kuvaa joho hilo wanadaiwa kukaidi.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Valerian Juwal, amesema kuwa uamuzi huo una baraka za wajumbe wa baraza hilo.

Baadhi ya madiwani wanaodaiwa kusimamishwa ni pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Frank Tarimo, Diwani wa Kata ya Ivaeny, Elia Kiwia, Diwani wa Kata ya Kirua, Robert Mrisho na Diwani wa Viti Maalumu Witness Riwa.

Wakuu wa wilaya watakiwa kufanya tathmini kwenye halmashauri zao
Marekani yadai China inajiandaa kuishambulia kijeshi