Madiwani watano wa vyama vya upinzani ikiwemo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), CUF na ACT-Wazalendo na viongozi wengine sita wamevikimbia vyama hivyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani.
 
Madiwani hao ni pamoja na Ramadhan Lutambi aliyekuwa diwani wa Kata ya Mailimoja kupitia Chadema na Ramadhan Kombe aliyekuwa diwani Kata Mbwawa kupitia ACT.
 
Wengine ni, Muharami Mkopi (CUF) Kata ya Ruaruke wilayani Kibiti, Seif Lwambo kupitia (CUF) Kata ya Beta, Muharami Mketo (CUF) Kata ya Lukanga na Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga.
 
Aidha viongozi waliojiuzulu kwenye vyama hivyo ni Ayubu Chapile ambae alikuwa katibu Kata ya Mkuza (CUF) ,Karimu Kasimu Katibu tawi chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere (Chadema), Selemani Mwinyimkuu mwenyekiti tawi (CUF), David Mramba ACT-Wazalendo, Latifa Sangalala mwanachama Chadema Mkoani B na Jumanne Urembo Diwani kivuli ACT-Wazalendo Kata ya Sofu.
 
  • Lema: Suala la haki, usawa na utawala wa sheria sio la Chadema peke yake
  • Video: Mjumbe wa CCM mkoa wa Simiyu afunguka hamahama ya Wapinzani
  • Vyama vya Upinzani vyasusia uchaguzi Tanga
 
Kwa upande wake, Ramadhani Lutambi amesema kuwa chama kinachofaa kuongoza nchi daima ni CCM kwani vyama vingine havina uwezo na havijali viongozi wa ngazi za chini.

Vitu 6 mwanaume wa kisasa anapaswa kuwa navyo
JKCI yasaini mkataba wa ushirikiano na Hospitali ya Moyo ya Fuwai