Kimbunga cha madiwani na wabunge kuhama hasa vyama vya upinzani na kuhamia CCM kimeendelea kutimka, ambapo jana usiku madiwani wengine wawili wa jiji la Arusha walifuata mkondo.

Madiwani hao walioshinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema, jana usiku walitangaza kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM hivyo kufanya idadi ya madiwani wa Arusha waliochukua hatua hiyo kufikia wanane.

Wakizungumzia sababu za kujiuzulu, Alex Marti wa kata ya Olasitin na Amani Liwadi wa kata ya Engutoto, wamesea lengo ni kumuunga mkono Rais John Magufuli.

“Nimeamua kwa ridhaa yangu mwenyewe kujiuzulu udiwani. Nimeandika barua kwa viongozi wa Chadema kueleza uamuzi wangu, kikubwa kilichofanya niamue hivi ni kazi nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli,” alisema Marti.

Liwadi pia alitoa sababu sawa na za Marti na kwamba tayari ameandika barua kwenda Chadema.

Uamuzi huo wa madiwani hao unaifanya Chadema kubaki na madiwani 25, huku madiwani wa CCM wakiwa saba kutoka idadi ya madiwani wawili waliochaguliwa mwaka 2015.

Arusha inatajwa kuwa ni moja kati ya ngome kubwa zaidi za Chadema.

Video: Naishukuru Chadema, Kalanga na hatuna ugomvi na Polisi- Fredy Lowassa
Video: Gari la watalii lapata ajali mbaya Arusha

Comments

comments