Malkia wa Pop duniani, Madonna amemtabiria mwanae aliyemuasili kutoka Malawi kuwa ni Rais wa nchi hiyo wa siku za usoni.

Madonna ametumia siku maalum ya sherehe zinazojulikana kama ‘Presidents’ day (siku ya marais) inayoadhimishwa nchini Marekani kila Jumatatu ya tatu ya mwezi Februari, kumtabiria mwanaye huyo mwenye umri wa miaka 12, David Banda.

“Katika siku ya Rais, nina sherehekea na Rais wa siku za usoni wa Malawi, moyo wa Afrika, Banda,” Madonna ametweet akiambatanisha na picha yao.

Madonna ana jumla ya watoto wanne aliowaasili kutoka Malawi, mmoja ni Banda, mwingine ni Mercy James na mapacha Stella na Estere.

Siku hii ilianzishwa mwaka 1885 nchini Marekani kwa lengo la kutambua mchango wa Rais George Washington. Serikali imeendelea kuitambua siku hii na kuiita ‘Washington’s Birthday (siku ya kuzaliwa ya Washington)’.

Takataka zaua watu 17, zazika nyumba
Watu 250 wauawa ndani ya saa 48

Comments

comments