Mwanasheria binafsi wa Rais wa Marekani, Donald Trump amekiri kumlipa kiasi cha Dola 130,000 sawa na zaidi ya Milioni 295 za Kitanzania nyota wa filamu za ngono aliyedai kuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Rais Trump

Mwanasheria huyo, Michael Cohen amesema malipo hayo kwa Mwanadada Stephanie Clifford maarufu kama Stormy Daniels yalikuwa halali ingawa amekana kutaja sababu za kumlipa fedha hizo.

Taarifa zinabainisha kuwa Rais Trump alijihusisha kimapenzi na Mwanadada huyo mwaka 2006,

Hata hivyo vyombo vya habari Marekani vimeripoti kuwa malipo ya fedha hizo yalifanyika mwezi Novemba, mwezi mmoja kabla ya uchaguzi kunyamazisha habari hiyo.

Kipindi anakabiliwa na shutuma hiyo mwaka, 2006 Trump alikuwa raia wa kawaida mwenye mke mmoja ajulikanae kama Melania na mtoto mmoja wa kiume ambapo kwa kipindi hiko alikuwa na miezi minne.

Malipo hayo kwa mara ya kwanza yameripotiwa mwezi uliopita na gazeti la Wall Street.

Trump mbele ya mwanasheria wake na mwanadada Clifford mwenye umri wa miaka 38, amekanusha kutokea kwa tukio hilo kati yao

Lakini mwezi uliopita gazeti la Celebrity lililotolewa 2011 katika mahojiano, Clifford ametoa taarifa hiyo  kwa urefu kuhusu mahusiano yake na Trump, na katika mahojiano hayo amesema alikutana na Trump katika uwanja wa kucheza golf mwaka 2006 ndipo walipokutana kingono.

 

Serena Williams arejea rasmi uwanjani
Habari Picha: JPM ashiriki Ibada ya Jumatano ya Majivu