Maelfu ya wananchi nchini Liberia wamefanya maandamano makubwa katika mitaa ya jiji la Monrovia wakipinga rushwa na kuporomoka kwa uchumi.

Waandamanaji hao wameitikia vuguvugu lililoanzia mitandaoni dhidi ya Rais Weah ambaye aliwahi kuwa mchezaji bora na maarufu duniani, wakimtuhumu kwa kushindwa vita dhidi ya ufisadi pamoja na ugumu wa maisha unaowakabili.

Waandamanaji hao ambao wengi wao walimpigia kura Weah mwaka 2017 waliweka kambi nje ya makaazi ya Rais. Baadhi yao walikuwa wamebeba mabango yaliyondikwa ‘traitor’ (msaliti).

Moja kati ya kashfa nzito zilizosababisha maandamano hayo kuwa na nguvu ya kuchapisha fedha ambayo ilisababisha nchi hiyo kupoteza $100 milioni zilizopaswa kuingia Benki Kuu, mwaka jana.

“Weah ameshindwa kutuongoza katika njia nzuri. Hali ya uchumi katika nchi yetu inazidi kuporomoka,”Reuters wanamkariri mmoja wa waandamanaji aliyedai alimpigia kura Weah.

Liberia ilikubwa na janga la Ebola mwaka 2014 hadi 2016, ambao ulichangia kuzorotesha uchumi wa nchi hiyo.

Jana, Serikali ya nchi hiyo ilifunga mitandao yote kwa kile lichotafsriwa kuwa ni jitihada za kutaka kuzima maandamano.

Mwalimu afariki baada ya kunywa gongo
Mambo yamnogea Pereira ndani ya Man United

Comments

comments