Imeelezwa kuwa Mafundi Sanifu ni kada muhimu katika maendeleo nchini katika ujenzi wa viwanda na ukuaji wa uchumi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho katika ufunguzi wa kongamano la tatu la mafundi sanifu lililofanyi mkoani Dar es Salaam.

Chamuriho amesema kuwa Serikali inatambua umuhinu wa mafundi Sanifu katika kufanya kazi na wahandisi na hivyo itaendelea kutoa kipaumbele kwenye vyuo vya VETA na vyuo vya ufundi ili kuhakikisha sera ya viwanda inakuwa endelevu.

“Serikali inatambua mchango wenu na na inawekeza kuhakikisha mnapata mafunzi hivyo ni wajibu wenu Mafundi Sanifu kuvitunza viwanda na miundombinu ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuchangia katika pato la taifa,” Amesema Chamuriho.

Aidha, Chamuriho ameongeza kuwa kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) viwango vya uwiano wa kazi za uhandisi ni 1:5:25 ambayo ni kila Mhandisi mmoja anafanya kazi na Mafundi Sanifu 5 na chini yao mafundi stadi 25.

Amesema kuwa kuanzia mwaka 2014 mpaka sasa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) imesajili mafundi sanifu 1,707 kati ya wahitimu 15,260 waliohitimu katika kipindi cha miaka kumi.

“Idadi hiyo ni ndogo hivyo nitoe wito kwa Mafundi Sanifu wote kujisajili kwani ni kosa la kisheria kufanya kazi bila kusajiliwa na bodi na pia kujikosesha haki zenu za msingi” amesema Dkt. Chamuriho

Aidha Chamuriho amewaasa Mafundi Sanifu wote kufanya kazi kwa weledi na uadilifu na kujiepusha na masuala ya rushwa ili kuisaidia Serikali kufikia azma yake ya kukuza uchumi.

Sambamba na hayo pia ameziomba Wizara na taasisi za Serikali kutoa kipaumbele kwa wataalamu hao kwa kuangalia muundo katika ngazi za utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kujali maslahi yao.

Mangungu: Yaacheni ya Haji Manara na Barbara
Okwi kutua Dar es salaam