Mvua iliyonyesha kwa siku tatu mfululizo wilayani kilwa mkoani Lindi imeacha zaidi ya wananchi 4500 wa vijiji sita bila makazi mkoani humo.

Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai amevitaja vijiji vilivyopata maafa hayo kuwa ni Kilanjelanje, Nanjirinji A Ruatwe, Njinjo, Nakiu na Nanjirinji B, ambapo amesema mbali na nyumba kubomoka mifugo mashamba ya wananchi hao navyo vimesombwa na maji

Ameongeza kuwa timu ya uokoaji imekwenda eneo lililokumbwa na mafuriko kwa boti kunusuru maisha ya Wananchi.

“Tunaendelea kuwaokoa na kuwapeleka maeneo ambayo tumeyatenga. Tunahitaji msaada wa chakula, dawa, nguo na vitu vingine muhimu,” amesema Ngubiagai.

Aidha amesema wananchi watapelekwa katika maeneo yaliyotengwa huku akiwataka watu wa kada mbalimbali kutoa msaada kwa Wananchi hao.

Sentensi 5 za Bryant zitakazoishi milele masikioni mwa watu
Orodha kamili ya watu 'wanane' waliofariki dunia wakiwa na Kobe Bryant

Comments

comments