Mafuriko ya maji yenye matope yameuwa watu nane katika kisiwa cha Majorca na wengine bado hawajapatikana.

Mafuriko hayo yametokea katika kisiwa cha Mashariki ya Uhispania baada ya mto kujaa matope la maji na kupasuka kutokana na mvua kubwa kunyesha.

Nyumba zimejaa maji na magari yamesombwa na maji hayo yenye tope yaliyo ingia mtaani na kwenye makazi ya watu.

Jeshi la nchi hiyo limewatuma kikosi cha watu 100 , mbwa, helkopta tatu na ndege ya kivita katika kisiwa hicho kutoka mji wa Valencia kwaajili ya kuongeza nguvu katika juhudi za uokoaji, na walio poteza makazi tayari wamepelekwa katika kambi kupata hifadhi.

Serikali za mitaa pia zimeandaa mpango wa kuongeza nguvu ya uokoaji.

Serikali kupitia waziri mkuu wa nchi hiyo Pedro Sanchez aliyetembelea eneo hilo imetoa pole kwa familia zilizo athirika na mafuriko hayo ya tope la maji.

Video: 'Beach' hatari zinazoweza kupoteza maisha yako papo hapo
Video: Dkt. Kihamia afunguka kuhusu uchaguzi wa marudio Liwale