Watu wasiopungua 31 wakiwemo wanawake na watoto, wamefariki baada ya mvua kubwa kunyesha Mkoa wa Parwan kaskazini mwa Afghanistan, iliyoambatana na mafuriko, huku wengine wapatao 100 wakiwa haijulikani walipo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Taliban, Bakhtar limesema mafuriko hayo yameharibu pia miundombinu huku shughuli za uokoaji zikiendelea ambapo tayari mashirika kadhaa yameelekeza misaada katika maeneo yaliyoathiriwa.

Bakhtar imesema, Mkoa wa Parwan ambao umezungukwa na milima na umekuwa mara kadhaa ukishuhudiwa kuwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa pia umeharibiwa na mafuriko hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yameleta madhara yanayohitajijitihada kiusaidizi.

Hata hivyo, Idara ya hali ya hewa ya eneo hilo imesema mvua zaidi zinatarajiwa kunyesha katika siku zijazo kwenye majimbo 34 ya Afghanistan, na kwamba mafuriko makubwa ya mwezi Juni na Julai kote nchini Afghanistan yamesababisha vifo vya watu 40.

Kenya: Wagombea walivyowasili Bomas tayari kwa matokeo
Mwisho wa 50 Cent na Mayweather wabainika