Takriban watu tisa wamepoteza maisha, na wengine zaidi wanahofiwa kufariki kufuatia kutokea kwa mafuriko katika mji wa Mbale mashariki nchini Uganda baada ya mito miwili kupasua kingo zake, na kufuata njia isiyo sahihi iliyoleta maafa.

Mamlaka za Serikali nchini humo, zimesema raia wengi wameyakimbia maeneo yao kwa hofu ya kudhurika na maji mengi yanayokatiza katika makazi yao, huku na wengine wakipoteza makazi yao baada ya maji kusomba nyumba waklizokuwa wakiishi.

Tayari, Jeshi la Polisi na Wanajeshi wameitwa kusaidia shughuli za utafutaji na uokoaji wa mali za raia katika eneo hilo la Mbale, ambapo wakazi waliokwama wanasema hawakuwa na jinsi ya kufanya isipokuwa kuokoa uhai wao huku wakishuhudia mali zao zikiharibiwa na kusombwa na maji.

Kamishna mkazi wa Mbale City, Ahamada Waashaki amesema Julai 31, 2022 miili tisa ilipatikana ambapo kati ya hiyo mmoja ni wa mwanajeshi.

Risasi yauwa wawili, 15 wajeruhiwa
Shule zafungwa kupisha uchaguzi Kenya