Magaidi 11 wameuawa, na wengine sita wamekamatwa wakati wa operesheni katika eneo la Tillabéri (magharibi), lililopo karibu na Burkina Faso, eneo ambalo ni la mauaji ya makundi ya kijihadi yanayohusishwa na makuAl-Qaeda na Islamic State.

Kupitia taarifa yake ya kila wiki, Wizara ya Ulinzi ya Niger imesema tukio hilo limetokea wakati wa moja ya operesheni iliyofanywa eneo la Doulgou ambapo magaidi hao walipouawa, pikipiki 13 kuharibiwa na silaha kukamatwa.

 Ulinzi katika barabara iliyo karibu na soko la Banibangou, lilolopo mji wa magharibi mwa Niger. Picha ya AFP.

Katika eneo la Gothèye, mashambulizi ya jeshiyamesababisha pia, kukamatwa kwa magaidi sita, pikipiki 125 na sehemu za vipuri vya pikipiki zilizoharibiwa, ambapo Wanajaeshi wawili walijeruhiwa miongoni mwa askari wa kikosi cha kupambana na jihadi cha Niger, Niya.

Kikosi hicho, kipo katika eneo hilo tangu Februari 2022, kikiwa na wanajeshi zaidi ya 2,000 huku tarifa za Jeshi zikisema wamesambaratisha mtandao wa magendo ya mafuta yaliyokuwa yakitumiwa na makundi yenye silaha, katika eneo la Torodi, lililoko kusini mwa Gothèye na Doulgou.

Polisi yafafanua taarifa za tishio la Ugaidi
Mabadiliko tabia nchi yanathiri uchumi wa Wananchi: Othman