Kiongozi wa kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo ni mshirika wa kundi la kigaidi linalojiita Islamic State of Iraq and Syria (ISIS), Abubakar Shekau ametuma ujumbe wa vitisho kwa Rais Mteule wa Marekani aliyeapa kuwafyeka magaidi, Donald Trump.

Kupitia kipande cha video kilichowekwa YouTube na kundi hilo la kigaidi lililojikita nchini Nigeria, Shekau amesema kuwa ndio kwanza vita imeanza dhidi ya mataifa ya Magharibi.

“Acheni kufurahisha kupitiliza na watu kama Donald Trump na mataifa yanayomuunga mkono duniani kupambana na ndugu zetu nchini Iraq, Syria, Afghanistan na sehemu yoyote,” anasikika Shekau katika ujumbe alioutoa kwa lugha ya Hausa.

“Tumemalizana na Obama, sasa tunaenda kuanza na Trump. Tunabaki imara na imani yetu na hatutakoma. Kwetu sisi, vita ndio kwanza imeanza,” aliongeza.

Ujumbe huo unaotafsiriwa kuwa ni wa kiuoga umekuja wakati ambapo kwa mara ya kwanza Marekani kupitia Trump imejipanga kushirikiana na Urusi kupambana na kundi la kigaidi linalojiita Islamic State of Iraq and Syria (ISIS).

Taarifa za uhakika zimeeleza kuwa Trump alizungumza kwa njia ya simu Rais wa Urusi, Vladmir Putin na wameahidiana kushirikiana katika vita dhidi ya kundi hilo la kigaidi ma makundi mengine.

Usain Bolt Kutua Signal Iduna Park Majira Ya Kiangazi
#HapoKale