Kundi la kigaidi la Al Shabaab limefanya mashambulizi ya mabomu kwa kutumia magari mawili yaliyosheheni vilipuzi,  karibu na makazi ya Rais wa Somalia na kuua watu 18.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la polisi nchini humo limeeza kuwa watu wengine 20 walijeruhiwa vibaya kwenye shambulio hilo.

“Magaidi walilipua mabomu karibu na ikulu, gari la mabomu lililipuka nje ya ikulu ambapo kulikuwa na wanajeshi wengi wakilinda mitaa inayoingia Ikulu,” alisema Abdikadir Abdirahman, Mkurugenzi wa kitengo cha Ambulances cha polisi.

Aliongeza kuwa washambuliaji waliuawa na wanajeshi wa nchi hiyo ingawa awali waliwaua kwa risasi wanajeshi waliokuwa kwenye kizuizi cha kuingia mtaa ulio karibu na makazi ya Rais.

Nao Al Shabaab wamekiri kuhusika na tukio hilo, wakijigamba kuwa waliweza kuwaua wanajeshi 15 kwenye mashambulizi hayo.

“Mashambulizi yalilenga makazi ya Rais na kitengo cha taifa cha ulinzi kinachoitwa Habar Kadija,” msemaji wa Al Shabaab, Abdiasis Abu Musab alisema.

Al Shabaab wana lengo la kuipindua Serikali ya Somalia ili waweke sheria katili za kiimani na kuigeuza nchi kuwa ya kidini.

Lissu amtaka Jaji Mutungi ajitafakari
NEC yakikaba koo kituo cha sheria LHRC