Watu wasiopungua 10 wakiwemo magaidi wanne wameuawa katika shambulizi dhidi ya soko la hisa la Pakistan, lililoko katika mji wa Bandari wa Karachi.

Kamanda wa polisi wa kanda, Sharjeel Kharal ameviambia vyombo vya habari kwamba walinzi wanne wa usalama, afisa mmoja wa polisi na raia mmoja ni miongoni mwa waliouawa.

Ameongeza kuwa magaidi wote wanne wameuawa na watu wengine saba wakiwemo askari polisi watatu wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.

Mkurungenzi Mtendaji wa soko la Hisa la Pakistan Farrukh Khan, amesema shambulio hilo lilikuwa zito, lakini kwa bahati nzuri magaidi hawakuweza kuingia eneo kuu la jengo la soko hilo.

Imeelezwa kuwa zaidi ya wafanyabiashara na wafanyakazi 1,000 walikwepo katika jengo wakati wa shambulio kwa mujibu wa ripoti.

Reli ya SGR kufika Mwanza, Arusha
Serikali yabainisha wanafunzi wasiotakiwa kuvaa barakoa