Gari mbili za mizigo, moja lenye namba za usajili Scania T182 DCM lililokuwa linatokea Iringa kwenda Dar es salaam zimegongana uso kwa uso eneo la Ruvu mkoani Pwani, na kutekea kwa moto.

Ajali hiyo imethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa ambapo amesema kuwa wakati tukio linatokea yeye alikuwa Kanisani hivyo atafutwe majira ya saa 7 mchana atakapokuwa ametoka kanisani ndipo atoe taarifa kamili.

“Wewe ndiyo unanipa taarifa kwa mara ya kwanza, kwa sababu niko kanisani itakuwa wasaidizi wangu wameshafika eneo la tukio, kwa hiyo naomba unitafute saa 7 mchana, nikiwa nimeshatoka kanisani na nitakupa taarifa kamili.” amesema RPC Wankyo Nyigesa.

Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia Dar24Media ili kuweza kupata matukio zaidi.

Singida United kuanza kutangaza usajili wake
Marekani yaanza mazungumzo na Wanamgambo wa Taliban

Comments

comments