Serikali imepanga kubadilisha matumizi ya baadhi ya magari yanayotumiwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kurusha maji ya kuwasha maarufu kama ‘Washawasha’ yaliyonunuliwa mwaka jana mwishoni kwa ajili ya kukabiliana na ‘fujo’, kuwa magari ya zima moto.

Akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga (Chadema), Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusuf Hamad Masauni alisema kuwa Serikali iko kwenye mchakato wa kuangalia uwezekano wa kubadili matumizi ya magari hayo ili yaweze kuongeza nguvu kwenye kitengo cha zima moto ambacho kina changamoto ya magari.

Serikali ilinunua magari 777 kwa bei ya kati ya shilingi milioni 150 na shilingi milioni 400, miezi michache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kati ya magari hayo, ni magari 50 pekee ndiyo yaliyotumika.

Young Africans Kurejea Dar es salaam Kesho
Zitto, Halima Mdee, Heche wahojiwa kwa kufanya fujo bungeni

Comments

comments