Kikosi cha Usalama Barabarani cha Shirikisho (FRSC), kimesema ajali iliyosababisha mlipuko wa lori la mafuta katika mji wa Ankpa uliopo jimbo la Kogi nchini Nigeria, umesababisha vifo vya watu wanane na majeruhi ambao idadi yao bado haijafahamika.

Kwa mujibu wa kamanda wa kikosi cha FRSC mjini Kogi, Stephen Dawulung amesema ajali hiyo ilihusisha Lori lililokuwa limebeba mafuta, basi la abiria aina ya yutong na magari madogo manne na pikipiki tatu na kusababisha vifo hivyo vinane.

Amesema, mashuhuda wa tukio hilo, wamesimulia kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya Lori kufeli breki ambapo walifanikiwa kuwaokoa watu wengine wawili wemye majeraha na kuwakimbiza Hospitalini kwa matibabu.

“Wafanyikazi wetu, ambao walikimbilia eneo la tukio, waliweza kuwaokoa watu wawili waliojeruhiwa na kuwakimbiza katika Hospitali Kuu, Ankpa, kwa matibabu ya haraka,” alisema Kamanda huyo wa kikosi cha FRSC.

Vyombo vya moto vilivyoungua katika moja ya tukio la ajali. Picha na Salemgisti.

Dawulung ameongeza kuwa, “Wasamaria wema, waliokota miili mingine minane ya wahasiriwa waliokuwa wameteketea kwa moto kutoka kwa magari na pikipiki kuungua kwa mafuta yaliyomwagika eneo hilo.

Hata hivyo, amesema kwa hali ilivyo sasa, hakuna uhakika na idadi halisi ya watu kwenye magari na pikipiki zilizohusika katika ajali hiyo ya kusikitisha na kwamba bado wanachunguza ili kujua takwimu halisi kwa ushirikiano na maafisa wa Chama cha Kitaifa cha Wafanyakazi wa Uchukuzi wa Barabarani, (NURTW).

Mambo matatu yaliyomuondoa Mzungu Simba SC
PICHA: Tembo Warriors waendelea kujifua Uturuki