Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imenunua mashine mbili maalumu zenye thamani ya Tzs. 245 Mil. ambazo pamoja na mambo mengine ndizo zitakazotumika kutoa huduma ya kupandikiza Uroto.

Mashine hizi zitasaidia kuvuna chembechembe mama za kuzalisha damu, Mazao ya damu ikiwemo chembe sahani, chembe nyeupe na Utegili.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya damu Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Stella Rwezaura amesema kwa hapa nchini mashine hizi zinapatikana Muhimbili pekee.

Akaunti za benki kufungwa nchini Guinea
Kesi ya Sabaya kusikilizwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi