Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Crescentius Magori, amewatuliza Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kwa kuwaambia watulie na kupuuza kinachoendelea kwenye mitandao ya Kijamii.

Magori amejitosa kuwatuliza Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo inayoshikilia Ubingwa wa Tanzania Bara kwa miaka minne mfululizo, kufuatia sauti (Clip) zinazoendelea kusambazwa mitandaoni kuhusu Muwekezaji Mohamed Dewji ‘Mo’.

Mjumbe huyo ambaye alikua mshauri wa ‘Mo’ kabla ya kujiuzulu nafasi ya uenyekiti mwezi uliopita, amesema kuna makusudi inafanywa kuivuruga Simba SC kwa kusambazwa kwa video hizo, hivyo Mashabiki na Wanachama wanapaswa kuwa watulivu na kuiamini klabu yao.

“Ukiona kuna Clip za hivyo zinamlenga mwekezaji wa Simba SC Tanzania, basi elewa ni kuwa hawa ndiyo wale wasioitakia mema Simba, msihadaike wanasimba!” ameandika Magori

Simba SC imekua kwenye taharuki kubwa baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana, Jumapili (Oktoba 24) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba SC yatolewa mbio za ubingwa 2021/22
Gomes aikana Young Africans