Rais John Magufuli jana aliwapa neema wananchi wanaopata huduma katika Hospitali ya Muhimbili na Kufifisha Shamrashamra ya misosi kwenye sherehe iliyoandaliwa kwa ajili ya kumpongeza baada ya kuagiza mamilioni yaliyochangwa kwa ajili ya sherehe hiyo yatumike kununua vitanda katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akiongea katika sherehe hiyo iliyoandaliwa kumpongeza yeye, Waziri Mkuu pamoja na wabunge baada ya kulihutubia Bunge hilo kwa mara ya kwanza Mjini Dodoma, rais Magufuli aliwataka waalikwa kuvumilia utofauti uliojitokeza kati ya sherehe walizozizoea na sherehe hiyo lakini wafurahi kuwa wamefanya tendo jema zaidi ya sherehe.

Rais Magufuli alisema:

“Inawezekana sherehe ya leo isiwe nzuri sana kuliko mlivyokuwa mmezoea, hakuna bia, kama kuna chupa za wine ni chache, megi ni maji na soda. Nilipoambiwa kwamba sherehe ya kujipongeza sisi wageni na wabunge katika kufungua Bunge la kumi na moja leo, nikawa nimetoa maelekezo kwa mheshimiwa Spika kwamba zile fedha zote zilizokuwa zimechangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya sherehe tuzielekeze katika masuala ambayo ni muhimu zaidi kuliko sherehe.

“Nimeambiwa kwamba zimechangwa karibu milioni 250, kwahiyo hizo fedha zote nilisema kama ni sherehe basi zitumike shilingi milioni 10 au milioni 15, zingine zikanunue vitanda vya hospitali ya Muhimbili. Kwahiyo nimeambiwa kwamba zaidi ya milioni 225 ndizo zilizokusanywa na kwenda kununua vitanda vya hospitali pale Muhimbili kwa kuwa wanalala chini. Tutakuwa tumejinyima sisi kwenye sherehe ya leo, lakini tutakuwa tumewasaidia wananchi ambao wanapata shida kubwa pale Muhimbili.”

Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimimbili na kubaini matatizo mbalimbali ikiwemo mashine za vipimo vya C-T Scan na MRI kutofanya kazi. Pia, alishuhudia wagonjwa wengi wakiwa wamelala chini (kwenye magodoro) kwa kukosa vitanda.

Jumba La Milioni 500 Lakumbwa Na Bomoabomoa Dar, Mmiliki Alia Na Kesi
Kylie Jenner achochea Kuni Taarifa za Kupigana Chini na Tyga