Mgombea urais kwa  tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli jana alifanya mkutano mkubwa unaosadikika kuvunja rekodi ya mikutano ya kisiasa iliyowahi kufanywa katika eneo la Tunduma ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa maono yake endapo atachaguliwa kuwa rais wa Tanzania.

Katika ahadi zake kwa wananchi, Dk. Magufuli aliahidi neema kwa walimu ambao alisema anafahamu vizuri kero zao kwa kuwa aliwahi kuwa mwalimu na mkewe pia ni mwalimu. Alisema endapo atachaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha walimu wanaishi maisha bora ikiwa ni pamoja na kujengewa nyumba bora na kuboresha mishahara yao.

Alisema kuwa walimu ni wito kama ilivyo miito mingine ya kiroho kutokana na kazi kubwa wanayoifanya hivyo ataboresha maisha yao ili na wao waishi maisha mazuri kama wachungaji wa kanisa katoliki (mapadri).

Tunduma

Dk. Magufuli pia hakuwasahau askari polisi katika ahadi zake ambapo alisema kuwa serikali hake itahakikiisha kuwa hali ya maisha ya polisi inaboreshwa ili wazidi kuipenda kazi yao. Alisisitiza kuwa atapambana vilivyo na mafisadi na wezi na kwamba mawaziri wake watafanya kazi kubwa ya kuahudimia wananchi bila kuchoka.

Magufuli alipata mapokezi makubwa ambapo maelfu ya wakazi wa Tunduma walikusanyika kumsubiri mgombea huyo kuanzia majira ya saa tano asubuhi huku ratiba yake ikionesha kuwa angewasili majira ya kati ya saa nane na saa tisa alasiri.

Mbatia Amtaka Kova Amkamate Mkapa
Misri Yajitoa All African Games 2015