Serikali ya Burundi kupitia ubalozi wake hapa nchini, imetoa mualiko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa kushiriki mazishi ya Rais Nkurunzinza yanayotarajiwa kufanyika Alhamisi tarehe 18 Juni 2020 nchini Burundi.

Hayo yamebainishwa wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro alipoenda kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini kufuatia kifo cha Rais wa Taifa hilo aliyefariki Juni 08, 2020.

Akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo
katika ubalozi ubalozi wa Burundi nchini, Dkt. Ndumbaro ametoa pole kwa wananchi wote wa Burundi na kuwasihi kuendelea kuwa watulivu na wastahimilivu wakati huu wa msiba.

“Kusaini kitabu cha maombolezo ni ishara ya ushirikiano wetu, umoja wetu na undugu wetu na ndugu zetu wa Burundi. Kifo cha Rais Nkurunzinza kinawahusu pia watanzania kwa sababu Rais Nkurunzinza ni Rais aliyekuwa karibu sana na Tanzania kuliko
nchi nyingine yeyote ile, lakini pia Burundi ipo karibu sana na
Tanzania, Amesema Dkt. Ndumbaro.

Naye Balozi wa Burundi nchini, Gervais Abayeho, amemshukuru Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro kwa kufika kwake kuhani msiba huo na kuongeza kuwa hali hiyo inaonesha upendo ambao unaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo
mawili.

Ngariba maarufu akamatwa Mara
OSHA watakiwa kuongeza nguvu, usimamizi sheria ya Usalama na Afya mahali pa kazi