Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. John Magufuli imeanza mchakato wa kuwashughulikia waliokisaliti katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Hiyo ilikuwa sehemu ya ajenda ya yaliyojadiliwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mwenyekiti wa chama hicho punde baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais mwaka jana.

Rais Magufuli aliahidi kuwashughulikia wasaliti wa chama hicho ambao hawakumfuata waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa alipohamia Chadema na kugombea chini  ya mwanvuli wa Ukawa, lakini walibaki wakiwa na ngozi ya CCM huku moyoni walikuwa wakimuunga mkono Lowassa na kuihujumu CCM.

Katika uchaguzi wa mwaka jana ulioshuhudiwa kuwa na ushindani mkubwa kuwahi kutokea tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, Rais Magufuli alishinda kwa asilimia 58.46 dhidi ya Lowassa aliyepata asilimia 39.97 huku akiviwezesha vyama vya upinzani kupata wabunge 116, idadi ambayo haijawahi kufikiwa na vyama vya upinzani nchini.

Sheikh Ponda ateta na Lema kwa dakika 60 gerezani, ampongeza kukaa mahabusu
Mchungaji: Nafahamu kuwa Dettol ni sumu lakini Mungu ameniagiza niwanyweshe