Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho Dkt. John Pombe Magufuli, ameanza rasmi kampeni zake leo Jumanne Septemba 1, 2020.

Magufuli ameanzia kampeni zake wilayani Bahi mkoani Dodoma ambapo amewaomba wakazi wa eneo hilo kumpigia kura ili aweze kupata ridhaa ya kuendelea kuwatumikia.

Ameahidi kufikisha umeme katika vijiji vyote 2600 vya Tanzania ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo.

Rais Magufuli pia ametumia nafasi hiyo kuwaombea kura wagombea wa ubunge wa baadhi ya majimbo ya mikoa ya Singida na Dodoma kupitia chama hicho na anendelea na kampeni zake sehemu mbalimbali za Tanzania.

Neema yavishukia vyuo vya kilimo nchini
Macron : Undeni serikali mpya