Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli jana aliwatahadharisha wanachama  wa chama hicho waloipinga kwa nyimbo katika mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) kukatwa kwa Edward Lowassa mwaka jana.

Baadhi ya wanachama wa chama hicho waliibuka na kuimba ‘Tuna imani na Lowassa’ katika mkutano wa NEC mwaka jana, dakika chache baada ya Kamati Kuu kulikata jina lake katika kinyang’anyiro cha kumpata mgombea urais wa chama hicho.

Akihutubia jana katika mkutano mkuu maalum wa chama hicho baada ya kukabidhiwa rasmi uenyekiti kwa kupigiwa kura za ndio na wajumbe wote, alisema kuwa angekuwa yeye ndiye mwenyekiti katika mkutano huo sehemu kubwa ya wanachama wangepotea siku ile.

“Nakumbuka siku ile wanaimba eti wana imani na mtu fulani, ningekuwa mimi ndiye mwenyekiti, robo au nusu wangepotea,” alisema.

Aidha, aliwaomba wanachama hao wamuombee ili aweze kuwa angalau na nusu ya uvumilivu aliokuwa nao Mwenyekiti Mstaafu, Dk. Kikwete.

“Nasema kwa dhati kabisa, Mheshimiwa mwenyekiti mstaafu, kuwa huo moyo wa uvumilivu ulionao, sidhani kama mimi ninao,” alisema.

Aliahidi kuwashughulikia wale wote wanaokihujumu chama kwakuwa ni bora kuishi na mchawi kuliko kuishi na msaliti.

Zitto ampongeza Magufuli, asema Wapinzani wana cha kujifunza CCM
Serikali ya Kenya yamtimua Koffi Olomide Kwa kumpiga mnenguaji wake wa kike