Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza kwa mara ya pili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo na kubaini changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na wagonjwa kuendelea kulala chini.

Akiwa katika wodi ya wazazi, Rais Magufuli alishuhudia idadi kubwa ya wagonjwa inayozidi vitanda huku akina mama waliokuwa katika wodi hiyo wakimueleza kuwa wanalazimika kulala zaidi ya watatu kwenye kitanda kimoja.

Magufuli, Muhimbili

Hali hiyo imedhihirika ikiwa ni miezi mitatu tangu Rais Magufuli alipoagiza mamilioni ya yaliyochangwa kwa ajili ya sherehe ya kumkaribisha Bungeni kutumika kununua vitanda katika hospitali hiyo, ambapo vitanda 300 vilinunuliwa.

Baada ya kuongea na uongozi wa hospitali hiyo kuhusu changamoto zinazowakabili pamoja na hatua nzuri waliyoipiga katika kuhakikisha wanakabiliana nazo, Rais Magufuli aliwaambia wananchi waliokuwa wakimsubiri nje ya hospitali hiyo kuwa amejifunza mengi kupitia ziara hiyo na atayafanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zaidi.

“Nimeiona hali halisi mwenyewe. Watu wanapata shida, watu wana mateso. Na ndio maana nimeamua kuja kwa makusudi sikuomba ruhusa hapa ili kusudi nijionee hali halisi ilivyo. Nimejifunza mengi, ninayabeba na najua namna ya kuyatatua. Mungu awabariki sana,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alitumia ziara hiyo pia kumtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zuberi ambaye amelazwa kwenye hospitali hiyo ya Taifa akipata matibabu, na alimfariji.

Magufuli na Mufti MkuuMagufuli na mufti mkuu 2

 

Ajabu: Mbuzi apewa dhamana baada ya kulala selo za polisi, ashtakiwa kwa kula mboga za bustani ya Hakimu
Tanzania Kuanza Na Shelisheli U-17