Rais John Magufuli juzi alifanya ziara ya kimyakimya na ya kushtukiza katika eneo la kivukoni jijini Dar es Salaam akiwa na walinzi wake wachache.

Taarifa zilizotolewa na mashuhuda wa ziara hiyo ambayo haikuhusisha vyombo vya habari zimeeleza kuwa Rais Magufuli alifika katika eneo hilo Jumapili majira ya saa 11 jioni akiwa na msafara wa magari matatu na kuingia katika moja ya ofisi.

Hakukuwa na king’ora chochote kama tulivyozoea bali ulikuwa ni msafara wa kimya kimya. Aliingia moja kwa moja kwenye zile ofisi na alitumia kati ya dakika 10 hadi 15 kabla ya kutoka,” Sharif Mkamba, mfanyabiashara ndogondogo katika eneo la kivukoni.

Mashuhuda walieleza kuwa inasadikika kuwa Rais hakumkuta mtumishi aliyekuwa ameenda kumuangalia katika ofisi hizo na baadae aliwasalimia baadhi ya wasafiri waliokuwa katika eneo hilo na kuondoka.

Vipande vya video zilizosambazwa kwa njia ya simu vinamuonesha Rais Magufuli akitembea kwa miguu katika eneo hilo la kivukoni. Hata hivyo, Mamlaka husika hazikupatikana kuelezea undani wa ziara hiyo ya kimyakimya ya Rais.

Profesa Lipumba ataka Magufuli atangaze mshahara wake, ajikate kusaidia
Ajabu: Mchezaji ampiga refa kadi nyekundu, angalia hapa video