Rais John Magufuli amesema kuwa kwa mamlaka aliyonayo kikatiba anaweza kubadili fedha za Tanzania ili watu waliozificha hivi sasa wakose mahali pa kuzipeleka.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika Mkutano wa 14 wa Wahandisi, uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa wapo watu ambao wamekuwa wakificha fedha zao majumbani kwao hali inayosababisha zisiingie kwenye mzunguko. Hivyo, amewataka watu hao kuacha mara moja tabia hiyo inayopelekea kukosekana kwa fedha kwenye mzunguko.

Rais Magufuli amewataka wananchi kufanya kazi kwani katika kipindi chake cha utawala ni vigumu kwa mwananchi asiyefanya kazi kupata fedha kwani awali fedha nyingi zilizokuwepo zilitokana na wizi serikalini.

Sebastian Nkoma Kuongoza Benchi La Ufundi La Kilimanjaro Queens
Taifa Stars Yaelekea Nigeria