Siku nne baada ya Rais John Magufuli kuahidi kuipa Kada ya Mahakama shilingi bilioni 12.3 ili kuisadia katika kutekeleza majukumu yake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ameikadhi kada hiyo hundi yenye kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi hiyo jijini Dar es Salaam, Dk. Mpango amesema kuwa Serikali inaamini kuwa fedha hizo zitaisadia mahakama kukamilisha kwa muda kesi zinazohusu ukwepaji wa kodi unaoikosesha serikali mapato makubwa.

“Kesi nyingi za kodi ambazo tunaamini zitakapoamliwa bila shaka… tunatarajia nyingi zitaamlia na zitasaidia upande wa serikali kupata mapato,” alisema Dk. Mpango.

“Baada ya kukabidhi fedha hizo, nieleze matumaini ya serikali. Mheshimiwa Naibu Katibu  Mkuu na Mtendaji wa Mahakama… Matumaini ya serikali ni kwamba fedha hizi zitatumika vizuri na zitatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa.

Rais Magufuli aliahidi kuipa kada ya Mahakama kiasi hicho cha fedha wakati akihutubia katika kilele cha siku ya Mahakama.

Mama Tunu Pinda ajeruhiwa katika ajali iliyomhusisha Bodaboda, mmoja afariki
Mawaziri wa Zamani waanza kutumikia adhabu ya kusafisha Hospitali