Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameendelea kusuka upya baadhi ya mashirika na makampuni ya umma ambapo leo amemteua Waziri Waziri Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu imeeleza kuwa Kindamba ameteuliwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Dkt. Kamugisha Kazaura ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Awali, Serikali ilianza kwa kuhakikisha inamiliki Kampuni hiyo kwa asilimia 100 baada ya kununua hisa zote za Bharti Airtel ambaye alikuwa mbia wa TTCL.

TTCL hivi sasa imetakiwa kujiendesha kibiashara na kuzingatia soko lenye ushindani wa mitandao mingine ya simu nchini.

JPM amteua Mhandisi Korosso kuwa Mwenyekiti ATCL
Daraja la aina yake kujengwa jijini Dar es salaam

Comments

comments