Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka shirika la umeme Tanzania (Tanesco) kuanza kufikiria kupunguza bei ya umeme, kwani sasa nchi inatarajia kuwa na umeme mwingi.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II, ambapo amesema kwamba kwa sasa miradi yote ya umeme ukijumlisha na wa Stiegler Gauge itafikia megawati 5000 , hivyo amesema ni wakati muafaka wa wizara husika kufikiria namna ya kupunguza bei ya umeme.

“Muanze kufikiria namna ya kushusha bei ya umeme, mmeanza vizuri muendelee na utaratibu huo. “Nchi ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme, maji , jua, upepo, makaa ya mawe, hata nyuklia, kwa sababu tunayo madini ya uranium yanayoweza kuzalisha umeme kwa nyuklia, kwa umeme wote huo hakuna haja ya kuwa na bei ya juu, ”amesema Magufuli.

Rais Magufuli ameendela kwa kusema kwamba nchi itakuwa na umeme wa kutosha, wa uhakika na kwa gharama nafuu, kwani hapo awali umeme ulikuwa ghali kutokana na umeme mwingi kuzalishwa kwa kutumia mafuta (dizeli). katika gridi ya Taifa.

Aidha Magufuli amewataka viongozi kuwa na mawasiliano baina yao ili kurahisisha maendeleo ya nchi kusonga mbele kwani katika hafla hiyo fupi ameonesha kukwaza na tabia ya viongozi kutokuwa na mawasiliano baina yao amesema.

Sasa niwaombe Mawaziri, Makatibu wakuu, Watendaji, wenye viti wa bodi msiogope kuwasiliana nyinyi kwa nyinyi hakuna sababu ya miradi mikubwa kama hii kuonekana inakwama kwasababu ya kukosa tu kibali cha TANROADS au kushindwa kupata kibali cha maji, kibali cha ardhi. Mimi mambo haya huwa nikiyasikia yananiudhi kweli labda nitumie lugha ya mjini mnaweza mkanielewa yananiboa kweli kweli”,

Hivyo ni wakati sasa wa viongozi katika sekta mbalimbali kushirikiana ili kuhakikisha miradi yote iliyozinduliwa na Rais John Pombe Magufuli inamalizika katika muda uliopangwa.

Miguna abanwa na sheria, atakiwa kuomba uraia upya
Tottenham kumzawadia Ponchettino Mkataba mnono.