Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa viongozi wa Manispaa ya Morogoro ambao wametumia fedha za  wafanyabiashara kwa kuwatoza gharama kubwa tofauti na utaratibu kuzirudisha fedha hizo .

Rais Magufuli ametoa agizo hilo Februari 11, 2021 wakati akizungumza na wafanyabiashara na wakazi wa Mkoa wa Morogoro mara baada ya kuzindua soko kuu la kisasa  la Manispaa ya Morogoro.

“Nilipoingia Soko la Manispaa ya Morogoro, nimepata ushahidi wa mtu mmoja, vizimba vinatakiwa kulipa  elfu 20 kwa Mwezi yeye anatozwa na mfanyakazi wa Manispaa anaitwa Haika, analipa  elfu 50 kwa Mwezi, Haika na wafanyakazi wengine kama wanapenda kazi pesa walizochukua wazitapike kuanzia leo,” amesema Rais Magufuli.

“Mkuu wa Mkoa Morogoro na DC Morogoro haiwezakani mambo ya ovyo yanafanywa na nyinyi mpo hapa, nyinyi ndio mnaniwakilisha Mimi,TAKUKURU kweli hamuoni hii rushwa?, kama  mfanyakazi wa Manispaa anakula Elfu 30 (cha juu) kila Mwezi kwa kutumia jengo la serikali hiyo sio rushwa?”  amesisitiza Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya Wafanyakazi wa Manispaa  hiyo kufanyia udalali majengo ya Manispaa kinyume na taratibu  na kukemea uozo uliopo Mkoani humo akiwaagiza Waziri wa TAMISEMI  pamoja Viongozi wa Mkoa huo kulishughulikia hilo upesi.

“Nataka uozo uliomo humu kwenye  Soko Kuu la Manispaa ya Morogoro kuanzia leo ukome, Waziri wa TAMISEMI, RC, DC, DED, Mbunge na wengine mkalishughulikie hili na nisilisikie tena, kama ni Elfu 20 hiyohiyo, nataka Wafanyabiashara wadogo wawe Mabilionea,” ameagiza Rais Magufuli.

Kocha Ibenge aingiwa hofu, amtaja Chama, Mkude
Mwinyi atumbua, ateua wapya