Serikali ya rais John Magufuli imeendeleza kasi iliyoanza nayo na hivi sasa imeonesha kuanza kuufanyia kazi kwa vitendo ujenzi wa barabara zinazopita juu (flyovers) jijini Dar es Salaam ili kuondoa adha ya foleni za magari.

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limeanza kufanya kazi ya kuhamisha nyaya za umeme zilizokuwa zikipita karibu na barabara katika maeneo ya uwanja wa ndege, karibu na kituo kidogo cha kuzalisha umeme cha Kipawa chenye KV 33.

Meneja wa Tanesco Mkoa wa kitanesco wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali amekieleza kituo cha runinga cha Star TV kuhusu utekelezaji wa zoezi hilo.

“Tumeanza wiki mbili zilizopita, na leo tumeshahamisha kwa asilimia 90. Baada ya wiki mbili tutawatangazia wananchi tutazima umeme tumalizie hii portion iliyobaki,” alisema na kuongeza kuwa baada ya hapo watahamia katika maeneo mengine.

Ujenzi wa flyover unatarajiwa kufanyika katika eneo la makutano ya barabara za Nyerere na Mandela na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 35.

Akiwa bado ni waziri wa ujenzi, Mwezi Oktoba mwaka jana, Dk. Magufuli alisaini mkataba wa ujenzi wa flyovers na kampuni ya kandarasi ya Sumitomo Mitsui Construction na aliahidi kuhakikisha ujenzi huo unatekelezwa kivitendo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Esther Bulaya Am-mwaga Wassira Mahakamani
Mwanasheria Mkuu Mstaafu amshauri Dk. Shein Kujiuzulu