Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdullaamesema aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ameliacha taifa likiwa salama na heshima kubwa sana.

Hayo ameyasema wakatik akihutubia wananchi wa Chato ambao leo wanaaga mwili wa Hayati Magufuli ambapo amesema kuwa Hayati Dkt. Magufuli aliaacha alama katika kila sekta hivyo hata siku moja haiwezi kutosha kuchambua jinsi alivyolitumikia taifa.

“Dkt. Magufuli ameliacha taifa hili likiwa salama na likiwa na heshima kubwa sana, tuliona alitutoa kwenye uchumi wa chini hadi uchumi wa kati kabla ya muda ambao ulitabiriwa na wataalamu na ni heshima kubwa sana heshima yake itaendelea kukumbukwa ni wajibu wetu viongozi na Watanzania tuungane kuyaenzi yale mazuri yote,” amesema Makamu wa wa Pili wa Rais Abdulla.

Ameongeza kuwa Hayati Magufuli alikuwa na maono makubwa hivyo hakuna mtanzania ambaye hajaumizwa na kusikitishwa na msiba huu mzito lakini kama bindanu inawapasa kukabiliana nalo na waweze kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele.

“Dkt Magufuli alikuwa na maono makubwa kiasi kwamba hakuna mtanzania mwenye akili timamu ambaye ndani ya damu yake, na ya mioyo yake hakusikitika na jambo hili kwa kweli ni jambo zito, lakini lazima kama binadamu tuweze kukabiliana nalo na tuweze mstiri na kumpeleka kwenye nyumba yake ya milele kwa heshima,” amesema Mhe. Abdulla.

Didier Gomes aitambia AS Vita
Blatter apigwa rungu jipya FIFA