Rais Dkt. John Magufuli amesema Serikali yake haiwezi kuendelea kuwalipa mishahara wafanyakazi waliokufa na walioacha kazi kama ambavyo ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali CAG ilivyobainisha.

Ameyasema hayo leo Machi 26,2020 wakati akipokea ripoti ya CAG na ya Takukuru, ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na kutolea mfano jeshi la polisi ambalo linaongozwa na IGP Simon Sirro aliyehudhuria katika makabidhiano hayo kuwa imebainika kuna polisi marahemu bado wanalipwa mishahara.

CAG abaini mapungufu CUF na CCM, fedha za ruzuku zatajwa

” IGP bahati nzuri yupo hapa…, Serikali hii haiwezi ikawa inalipa mishahara ya watu waliokufa kwa taasisi muhimu kama ya Polisi wakati ‘luckup’ mnazo ninyi, pingu mnazo ninyi, mmeshindwaje kuwashika hawa  wanaohusika na kuwaweka huko, kwanini mnawazunguka, mnashika huku wengine mlionao hapo hapo mnashindwa kuwashika?” Ameuliza rais Magufuli.

Amesema jeshi la polisi ametolea mfani tu, lakini kuna taasisi ambazo zimefanya vibaya zaidi na uongozi chini ya waziri mkuu wataifanyia kazi ripoti hiyo huku ikipelekwa bungeni mapema…,Bofya hapa kutazama.

Brg. Jenerali wa Takukuru apandishwa Cheo kwa kuokoa mamilioni
CAG abaini mapungufu CUF na CCM, fedha za ruzuku zatajwa

Comments

comments