Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Tano, John Pombe Magufuli, leo katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha kufua umeme Kinyerezi ii, amefunguka na kudai kuwa anaukubali sana wimbo wa ”Hawawezi Kushindana” ulioimbwa na msanii wa muziki wa injili, Goodluck Gozbert.

Katika wimbo huo Godluck ameimba maneno kuntu yaliyo wagusa watu wengi akiwemo Rais Magufuli ambapo mara baada ya kupigwa wimbo huo Magufuli amejikuta kushindwa kuzuia hisia zake na kutaka wimbo huo kupigwa tena kwa mara ya pili akionesha ni jinsi gani anaukubali wimbo huo.

Rais Magufuli amesema ”Naomba niseme tena kale kawimbo kamenigusa sana, naomba kachezwe tena hapa ” .

Goodluck Gozbert ni moja kati ya wasanii waliokuja kwa kasi sana katika muziki wa injili na kuinua vipaji vya watu wengi katika sanaa hiyo ambayo hapo awali wasanii kama Rose Muhando walikuwa wakivuma sana na nyimbo za injili kwa namna yao.

Gozbert amefanya mabadiliko makubwa katika muziki wa injili na wimbo uliompatia umaarufu zaidi ni  wimbo wake wa ”Ipo siku”, ni moja ya wimbo uliogusa watu wengi kwa namna mbalimbali ukiwatia moyo juu ya mafanikio yao kuwa wasikate tamaa kuwa ipo siku watafanikiwa.

Hawawezi kushindana ni moja ya truck iliyotolewa hivi karibuni na ni moja ya truck za nyimbo za injili zinazoyofanya vizuri.

Kuitazama nyimbo hiyo bonyeza linki hapo chini.

 

Breaking news: Mbowe, viongozi wenzake waachiwa kwa dhamana
Masogange ahukumiwa kifungo jela

Comments

comments